Utangulizi.
Tangu awali kumekuwepo hadithi, mafumbo,methali na vitendawili kutoka kwa mababu zetu,mafumbo,vitendawili,methali na hadithi vilikuwa si tukio halisi,yalielezea kwa uficho ili mtu aweze kujifunza,au mtu aweze kufumbua fumbo au methali na vitendawili hivyo,ambavyo vilikuwa ni lugha ya ishara,au kivuli lakini kitu halisi kilitokea baadaye.pamoja na hayo tutaongelea juu ya; kuonyesha uhalisia wa lugha na ishara zilzotumika kuelezea imani ya kikristo kupitia kwa barua kwa makanisa saba,tutatumia vitabu vya kitheologia na mawazo yetu.
Uhalisia maana yake ni kuonyesha kitu halisi badala ya ishara au picha ya mtu,ni kufunua jambo ambalo ni la kweli,ni kufahamu au kuona kitu chewnyewe.Uhalisia utumika kuelezea lugha na ishara,imani ya kikristo kwa barua kwa makansa saba ''makanisa yalitajwa ni makanisa saba ambayo yalikuwepo wakati wa Yohana, katika kuyashughulikia, aonekana anatutolea historia fupi ya makanisa kutoka kanisa la karne ya kwanza hadi kanisa la siku hizi katika vipindi saba, makanisa hayo saba yalikuwa ni Kanisa la Efeso, Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.
''Kanisa la Efeso ni kanisa la upendo wa kwanza,ni kanisa la Mitume [uf.2;1-7]'1.Ni kanisa lililofundishwa uongo juu ya vyakula vilivyotolewa sadaka za miungu kwa kushiriki matendo ya zinaa, Paulo anaonya kuwa warudie hali ya kiroho ya upendo. Ufunuo unaonyesha kuwa Roho atawalaye makanisa ataendesha hukumu [uf.2;4-6].Na washindao watafurahia ukamilifu wa uzima wa milele katika ulimwengu ujao.
Kanisa la Smirna ni kanisa lenye mateso wakati wa 'Deocletian' mpaka wakati mfalme Constatino [uf. 2;8-11] mfalme Constatino alipigana vita na kushinda,kabla ya vita aliona alama ya MSALABA. Ilikuwa mwaka 312 AD. Mashambulio hayo ya mateso, kanisa Smirna walikuwa maskini wa mali lakini ni tajiri wa kiroho, walifungwa gerezani mashambulio na mateso yatadumu milele,Mwokozi wao Yule aishiye milele, alishinda mauti [uf.1;18,2;8].Hatairuhusu mauti iwaguse roho zao. Katika yeye wana wa ushindi wa uzima wa milele [uf.2;10-11].
Kanisa la Pergamo ni kanisa lililokuwa chini ya upendo wa kifalme
chini ya mfalme Constatino [Ufu. 2;12-17].Ambapo Mfalme Cnstatino wakristo walishuhudia, walihubiri waziwazi, walijenga makanisa, na kuishi maisha ya kikristo yenye upendo zaidi bila wakristo kogopa. Mfalme aliliweka kanisa katika AMANI wakati wake, [mwaka 500 BK]
Kanisa la Thiatra ni kanisa la papa, wakati wa giza kuu [uf.
2;18-19]. Kanisa liliabudu wafu,mfano Mariam mtakatifu,watakatifu wengine,picha,[Yelcs] au taswira. Papa walitengeneza tiketi za msamaha wa dhambi [Indulgence].Viongozi wa makanisa walijiingiza kwenye mambo ya anasa,ulevi,wakawa na vimada,watumishi walishindwa kuogopa maadili ya kanisa, hawakufuata MAANDIKO MATAKATIFU [BIBLIA]
Kanisa la Sardi, ni kanisa la uprotestanti, matengenezo ya kanisa katika karne ya 16 na 17, [uf.3.1-16] watu wa kiprotestanti walileta matengenezo kupinga kanisa la Papa,na kanisa Thiatra na baadhi ya taratibu wazojiwekea.
Kansa la Filadelfia, ni kanisa la wapelekwa [wamissionary] wakati ulionyeshwa kwa njia ya ushirika wa watawa [monks] wamonki, [uf.3.7-13] .Ni watu walioishi kwa kujitega na ulimwengu katika karne ya 4.
Kanisa la Laodikia, ni kanisa lililokaririwa, kanisa la uasi wa mwisho [uf.3.14-19]. Kanisa hili ni kanisa ambalo ni la uasi, ambalo lilifanya dhambi, watu walijivunia elmu yao wakamsahau MUNGU. Kanisa la Laodikia ndilo kanisa la sasa, kanisa la uasi, watu wamejivunia elimu yao na kumsahau MUNGU. Makanisa haya yalikuwa ni kivuli au ishara, picha, lugha, inayoonyesha uhalisia wa makanisa ya mwanzo,wakati wa Papa na wakati huu wa karne ya 21. Kwa hiyo kanisa ni mtu mmoja mmoja, YESU anabisha hodi kwa kila mtu atakayemfungulia ataingia mwake . Tumfungulie mioyo yetu aingie awe pamoja nasi.[uf.3.20].
NUKUU;
1; Mears c. Henrieta, mambo Biblia ifunzayo 2,[Inland Publishers 1995, Mwanza, Tanzania] uk 223.
2; Fleming, Don Biblia inasema,kanisa la Biblia KLB,2ooo,Dodoma Tanzania] uk 685.
Walioandaa; Kundi na 1.
- L. Musirimu
- Solomon O. Bukwe
- Hosea F.Chamba
- Stephen J. Kassanda.
MAONI YA MWALIMU
1. Kazi mmefanya kubwa sana
2. Ni vyema kuelewa na kujibu moja kwa moja hitaji la swali.
3. Mlitakiwa kujadili lugha za picha na ishara pekee na jinsi zinavyoweza kulifaa kanisa leo.
4. Uchapaji wa kazi sio mzuri (najua shida ilipo) ila fanyeni mazoezi mengi zaidi
5. Alama
65%
No comments:
Post a Comment