Monday, June 20, 2011

MTAALA WA MASOMO: BUNDA BIBLE COLLEGE


IT101 UTANGULIZI WA KITARAKIRISHI
Katika kosi hii mwanachuo atajifunza utangulizi wa utumiaji wa Kitarakirishi, vile vile atajifunza vyanzo vingine kielektroniki (kama vile Internet) kwa ajili ya kumsaidia kuandika, kutunza na kufanya utafiti wa kimaktaba.

Mwisho wa kozi mwanachuo atakuwa na uwezo wa:
·         Kuelewa sehemu za kitarakirishi: hardware, software na peripherals
  • Kutumia programe mbalimbali kwa usahihi
  • Kutumia mbinu mbalimbali za kitarakirishi katika kufanya utafiti

Mambo muhimu kwa mwanachuo kufanya katika kozi hii
Mwanachuo anatakiwa kuhudhuria na kushiriki katika jumla ya vipindi 60 kwa mwaka mmoja. Kila semester mwanachuo anatakiwa kukamilisha vipindi 30
Kila semester aandike insha mbili: moja binafsi na nyingine kwa makundi ambayo itawakilishwa kwenye semina kabla ya kukusanywa kwa mkufunzi.
Mwanachuo atafanya majaribio yasiyopungua mawili kwa kila semester

MADA
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
IT101
Msingi wa Kitarakirishi

a)    Utangulizi wa Kitarakirishi
Mwanachuo aweze kueleza;
1.    Maana ya kitarakirishi
2.    Kutaja aina za vitarakirishi na matumizi yake
3.    Sehemu za ndani na nje ya kitarakirishi
4.    Mazoezi ya uchapaji (keyboard practice)
Mkufunzi awaongoze wanachuo
1.    Kujadili, kueleza na kutaja aina na sehemu za Kitarakirishi.
2.    Kuunganisha, kuwasha na kuzima kitarakirishi.
3.    Kutumia Keyboard


Je wanachuo wanaweza kuwasha na kuzima kitarakirishi kwa usahihi na kuchapa?
15
 b) Utumizi wa Kitarakirishi
Mwanachuo aweze;
1.    Kutumia Window: File na Folder, kuchapa, kufuta, kutunza na kufunga.
2.    Kutunza kazi katika BackUps devices.
Mkufunzi awaelekeze wanachuo kufanya mazoezi kwa vitendo na nadharia
1.    Kujadili maana ya window, file, folder, kuchapa, kufuta, kutunza, kufuta, na kufunga.

Je, wanachuo ni mahili kueleza na kutumia kitarakirishi katika eneo walilojifunza?
15
 IT111
UTUMIZI WA KITARAKIRISHI







c)  Ufahamu wa Word Processor


Mwanachuo aweze kueleza:
1.    Kutaja sehemu za Menu ya window, screen tips, File menu na yaliyomo
2.    Kutumia Edit menu (copy, paste, select all, do na undo, cut)
3.    Kutumia Insert menu (page break, footnote, na options)
4.    View menu (header/footer, page layout)
5.    Kutumia format menu (styles)
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:
1.    Kujadili matumizi ya window menu
2.    Kufanya mazoezi ya namna menu zitumikavyo
3.    Kutengeneza chapisho na kisha kuingiza mitindo mbalimbali kama Font, paragraph, bullets and numbering, border nk.


Je, wanachuo wana uweredi wa kutosha katika matumizi ya word processor?
20
d) Tovuti





Mwanachuo aweze:
1.    Kueleza maana ya Tovuti na faida zake.
2.    kutaja njia za  kutumia Internet
3.    Kufungua anuani (e-mail address), kuandika barua barua pepe, kuambatanisha na kutuma
4.    Kutumia Google kama chanzo cha taarifa na vipeperushi katika kufanya utafiti
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:
1.    Kujadili na kueleza maana ya tovuti, faida na hasara katika maisha ya kanisa
2.    Kutumia tovuti kuwasiliana
3.    Kutumia Google katika kufanya utafiti
4.    Kufungua anuani ya barua pepe.



Je, wanachuo wanaweza kutumia ipasavyo tovuti katika kujisomea na kuwasiliana?

Je, wanachuo wanamtazamo gani juu ya umuhimu wa matumizi ya tovuti ndani ya kanisa?
10


RS100 DINI MBALIMBALI
Kosi itampatia mwanachuo utangulizi wa dini katika vipindi tofauti ndani ya miaka mitatu. Kujifunza asili na mikazo ya dini husika.

Mwisho wa kozi mwanachuo atakuwa na uwezo wa:
·         Kufafanua asili na historia ya dini alizojifunza
·         Kuonyesha uwelewa wa kimawazo na vitendo dhidi ya mtazamo wa kidunia juu ya dini alizosoma
·         Kuchambua kimantiki mafundisho ya dini hizo dhidi ya theologia ya kikristo na kuonyesha imani ya Kikristo ndiyo iliyo bora kupita zote
·         Kufanya mazungumzo au uinjilist na watu wa imani tofauti na kuwafanya kuwa wakristo.

Mambo muhimu kwa mwanachuo kufanya katika kozi hii
Mwanachuo anatakiwa kuhudhuria na kushiriki katika jumla ya vipindi 90 kwa miaka yote mitatu. Kila semester yenye kozi hii mwanachuo anatakiwa kukamilisha vipindi 45
Kila semester aandike insha mbili: moja binafsi na kazi ya kikundi ambayo itawakilishwa kwenye semina kabla ya kukusanywa kwa mkufunzi.
Mwanachuo atafanya majaribio yasiyopungua mawili kwa kila semester na mtihani wa mwisho kwa semester hiyo.


MADA
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
RS100
UTANGULIZI WA DINI MBALIMBALI
a)      Mitazamo ya Kiimani duniani:
·         Dini za Asili za Kiafrika.































Mwanachuo aweze:
1.      Kuelezea asili na mafundisho ya kila mtazamo wa DAK waasisi, mtindo wa kuabudu, ushirikiano, uenezaji wa dini na kulinda imani ya katika DAK.
2.      Kutaja na kuelezea changamoto mbalimbali dhidi ya ukristo
3.      Kujadili mchango wa DAK katika ukuaji au kudhoofisha ukristo Afrika.
4.      Kuchambua mbinu mbali mbali zenye kumwezesha mtumishi katika kufikisha Injili na kuwaongoa wafuasi wa DAK.
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kutambua asili ya imani au utambuzi wa Mungu katika kabila la mwanachuo.
2.      Kujadili kitaaluma mafundisho juu ya DAK
3.      Kutumia uzoefu wao kuchanganua mabaki ya imani za DAK na jinsi zinavyo athiri Ukristo
4.      Kupendekeza njia anuwai za kuwafikishia Injili waumini wa DAK
5.      Kulinganisha mafundisho na kujithibitishia ubora wa imani ya Kikristo

Je, wanachuo wanafahamu asili za imani za watu wa bara hili (Afrika)?

Je, imani za DAK zinaathiri kwa namna gani imani ya Kikristo na huduma ya kanisa kwa ujumla?
45
RS110 MITAZAMO YA KIIMANI DUNIANI
b)     Uislamu
Mwanachuo aweze:
1.      Kuelezea asili na mafundisho ya kila mtazamo wa Uislamu , mwaasisi, mtindo wa kuabudu, ushirikiano, uenezaji wa dini na kulinda imani ya dini husika.
2.      Kutaja na kueleza madhehebu ya ya Uislamu
3.      Kutaja na kuelezea changamoto mbalimbali dhidi ya ukristo
4.      Kujadili mchango wa dini hizo katika ukuaji au kudhoofisha ukristo duniani
5.      Kuchambua mbinu mbali mbali zenye kumwezesha mtumishi katika kufikisha Injili na kuwaongoa wafuasi wa dini hiyo.
1.      Kutambua asili ya imani au utambuzi wa Mungu katika kibila la mwanachuo.
2.      Kujadili kitaaluma mafundisho juu ya DAK.
3.      Kutumia uzoefu wao kuchanganua imani na mafundisho ya Uislam na jinsi zinavyo athiri Ukristo.
4.      Kupendekeza njia anuwai za kuwafikishia Injili waumini wa Uislam.
5.      Kulinganisha mafundisho na kujithibitishia ubora wa imani ya Kikristo

Je, wanachuo wanaweza kueleza msingi wa imani ya kiislamu na kuweza kuitetea imani ya Kikristo mbele ya waislamu.


45



































TS100 STADI ZA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHIA
Mwisho wa kosi hii mwanachuo atakuwa na uwezo wa:
·         Kujiandalia na kufuata ratiba yake mwenyewe ya kimasomo
·         Kusoma na kutengeneza notisi kutoka kwenye vitabu, majalida na magazeti
·         Kutumia vyanzo mbalimbali vya habari katika kujifunza na kufundishia
·         Kuchambua kwa ufasaha yaliyomo na maudhui ya kitabu
·         Kuandika kazi mradi (essay) kitaaluma
Mambo muhimu kwa mwanachuo kufanya katika kozi hii
Mwanachuo anatakiwa kuhudhuria na kushiriki katika jumla ya vipindi 90 kwa mwaka mmoja. Kila semester mwanachuo anatakiwa kukamilisha vipindi 45
Kila semester aandike insha mbili: moja binafsi na nyingine kwa makundi ambayo itawakilishwa kwenye semina kabla ya kukusanywa kwa mkufunzi.
Mwanachuo atafanya majaribio yasiyopungua mawili kwa kila semester, na mazoezi ya kufundisha wenzake (kuongoza mtaala kwa mazoezi ya vitendo)
Mwanachuo ataendelea na kozi nyingine baada ya kufaulu vyema kozi tangulizi kwa zaidi ya 50% ya kazi zote za darasa


MADA
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
TS100
Uandishi
Kuchukua na kutengeneza notisi
Mwanachuo aweze:
1.      Kusikiliza kwa makini maelezo ya mkufunzi darasani
2.      Kuandika mhtasari wa maelekezo ya mkufunzi
3.      Kusoma vitabu na kujitengenezea notisi
4.      Kuandika insha kwa kufuata kanuni za kitaaluma
5.      Kuatumia Kiswahili fasaha katika
kuandika isha za kitaaluma
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kujua umuhimu wa stadi ya uandishi na aina zake
2.      Mbinu na mazingira ya kusikiliza na kuchukua notisi awapo darasani
3.      aina mbali mbali za kutengeneza notisi za kitaaluma
4.      Uandishi wa insha ndefu, mambo ya muhimu kati insha, mitindo mbalimbali ya uandishi wa insha.
5.      Kujifunza Sarufi sanifu za Kiswahili (Kundi la maneno – speech of words)

Je, wanachuo wanaweza kujitengenezea na kuchukua notisi kama wanavyosikiliza na kujisomea vitabu?


Je, wanachuo wanaandika insha kwa kanuni za matumizi ya lugha ya Kiswahili na kufuata kanuni za uandishi wa insha?
45
TS110
Elimu ya Kikristo
a)      Historia ya Elimu ya Kikristo
Mwanachuo aweze kueleza;
1.      Maana na uasisi wa Elimu wa Kikristo
Mkufunzu awaongoze wanachuo kujadili na kueleza maana ya Elimu ya Kikristo.
Pia kufundisha hatua ya historia ya E.K

Je wanachuo wanaweza kueleza maana na historia ya E.K?
45

b)      Vitengo vya Elimu ya Kikristo
2.      Kutaja walengwa wa E.K na sababu zake
Mkufunzu awaongoze wanachuo kujadili na kufanya utafiti kwa kutumia uzoefu wao juu ya Sunday school, TAYO, UMAKI, UBAKI, Bible studies, vyuo vya Theologia n.k

Je, mwanachuo anaweza kutoa na kusimamia EK katika makundi mbalimbali yaliyomo kanisani kwake?


c)      Utangulizi wa Falsafa ya Elimu
Mwanachuo aweze kueleza:
1.      Maana ya Falsafa ya Ualimu
2.      Misingi na Mafilosofia wa E.K
3.      Aina za elimu
Mkufunzi awaelekeze wanachuo
1.      Kujadili wanafalsafa ya Elimu.
2.      Kuelezea wanafalsafa wane: zingatia wanafalsafa wa kiafrika. (J.K Nyerere)
3.      Kueleza elimu kabla na baada ya ukoloni

Je, mwanachuo aweza kujenga falsafa yake binafsi katika kutekeleza ajenda ya Elimu ya Kikristo?


d)      Utangulizi wa Saikolojia ya Elimu
Mwanachuo aweze:
1.      Kueleza maana ya saikolojia, asili yake, matawi yake na mabingwa wa saikologia ya Elimu
2.       Maana ya saikolojia ya Elimu
3.      Athari za Ukuaji na akili
4.      Kutambua makundi
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:
·        Kujadi na maana ya saikolojia  na matawi yake yote na jinsi yalivyo na uhusiano na saikolojia ya ELimu
·        Kuchimbua mabingwa wa  saikolojia ya Elimu na kujadili mitazamo yao.
·        Kuchungua athari zitokanazo na mazingira jinsi zinavyoweza kutoa mchango katika maendeleo ya ukuaji akili
·        Kujadili mbinu za kusaidia wanafunzi kushinda hali dhaifu katika kupokea maarifa mapya.



Je, mwanachuo anaitumia saikolojia ya Elimu katika kutoa elimu hitajika kwa makundi yanayohitaji ujuzi wake?


e)      Kuandaa Mtaala na kufundisha
Mwanachuo aweze:
1.      Njia sahihi na viwango katika uandaaji wa mtaala wa biblia kwa kuchambua mada na kuwasilisha
2.      Kutumia mbinu sahihi kufundishia
3.      Kutumia njia sahihi za tathmini ya kazi ya mtaala
4.      Kuandaa taarifa ya darasa
Mkufunzi amwongoze mwanachuo:
·        Kujadili maana na umuhimu wa mtaala (Bible study), n.k
·        Kuonyesha namna mbalimbali za uandaaji wa mtaala na mbinu za kufundishia mtaala huo kwa makundi mbalimbali ya wanafunzi.
·        Kutumia mtaala rasmi na kuuchambua katika mada kuu, mada ndogo, malengo yake na viwango vya wanafunzi
·        Kuandaa taarifa za tathimini kila kabla, wakati na baada ya kumalizika kwa mtaala. Na kujua faida zake


Je, mwanachuo anaonyesha uweredi katika kuandaa mtaala kuongoza Bible Study na kuusimamia?
































LL106 ENGLISH
This course will introduce the language use with the ultimate aim of equipping you with skills in speaking and writing as well as ability to translate and preaching simple Bible texts.

At the end of this course you should be able to:
·         Addressing in English correctly
·         Constructing academic assay
·         Identifying the significance of mood, tense, case, gender, etc for translation
·         Make effective use of tools for research (concordances, grammars, dictionaries, etc)
·         Preparing simple sermons and presenting with and without notes

Course requirements:
A student should attend all courses’ sessions for three years. No any accuse for absentees
The course has total of 3 units with 270 periods for three years.
A student is required to complete all given assignments and tests on time.


TOPIC
SUB TOPIC
LEARNING/TEACHING OBJECTIVES
LEARNING/TEACHING STRATEGIES
TEACHING/LEARNING AIDS
REFERENCE
No. OF PERIOD

INTRODUCTION
Orientation
A student should be able to:
·         Mention by writing and pronounce the alphabets in order form
·         Counting number 0 – 50
·         Building classroom objects and activities vocabularies (color, chairs, window, learn, read, teach (etc)
·         Mention things and activities done at home (sleep, work, cook, wash, bath, care, room, bed, farm, cultivate etc)
·         Mention cities, nationalities.
Both student and tutor should be able to:
·         List all alphabets in proper order and distinguishing the consonants and vowels.
·         Make use word formation to create different vocabularies which express activities done at home, church and school
·         Prepare cards for learning values
·         Use those numbers to read chapters and verses in the Bible.






Expressing Everyday Activities
A student should be able to;
·         Use key words to express his/her every activities done individually and in groups: often, always, (at home and school)
·         Describe things (It, cat, buildings
·         Use different form of sentences to construct grammatical sentences (interrogative, statement, affirmative)
Student and tutor should be able to;
·         Clarify and use different activities that expressed by everyday activities (simple tenses)
·         A tutor should start with simple present, past simple, future simple tense and leads a lot of drills, orally and writing. E.g. I am a student, I was a student, I will be a student





ENGLISH STRUCTURE
Expressing ongoing activities
A student should be able to;
·         Use key words express ongoing activities: am, is, are, were, and was with the addition of ING at the end of a verb.
·         Describe people and things activities (at home, church and school)
·         Use different form of sentences to construct grammatical sentences (interrogative, statement, affirmative)
Student and tutor should be able to;
·         Elucidate and use different activities that expressed by ongoing activities (progressive tenses)
·         A tutor should start with present, past, future simple tense and leads a lot of drills, orally and writing. E.g. I am going, I was going, I will be going.






Self -Introduction
A student should be able to;
·         Tell about himself or herself both orally and written
·         Introduce other students orally.
A student and a tutor should be able to;
1.        Guide students to apply all tenses taught in their description.
2.        Help them to make brief explanation about their vocation and other fellows





Word speech
A student should be able to:
·         Understand and be able to use all types of word speech
·         Make sentences orally and writing
·         Using tenses, places, manner, quality in different sentences.
·         To construct grammatical English sentences
A tutor should lead student to:
·         Describe the use of each type in word speech
·         Prepare teaching aids esp. card
·         To take all structural in their daily communication
·         Using the types of sentences to construct orally and written sentences.





Writing skills
Punctuation
A student should be able to:
·         To use proper punctuation marks within a sentences
·         To punctuate a given composition
·         Writing a short story form the Bible
A tutor should lead the students to:
·         Discuss the use of punctuation marks and use them in writing skills
·         To write personal story
·         Paraphrasing a short Biblical stories





Letter writing
A students should be able to:
·         To draw a friendly and Business letters’ format
·         To address his/her feeling personally through friendly letter
A tutor should organize the students to
·         Discuss the meaning and the importance of letters, types and format of both types.






Developing paragraphs
A student should be able to:
·         Understand the procedures of developing paragraphs
·         To write an essay contains several paragraphs
A tutor should provide
·          










Listening and Speaking
Interview
A student should be able to:
·         Interview one another
·         Listening to exercise, greeting people, listening exercise
·         Conducting simple conversation meeting
A tutor should conduct
·         Interview sessions for students to interview themselves.
·         Guide students to listen and speak to each other
·         Preparing several drills to facilitate listening and speaking
·         Debates, discussions and dictation




Reading skills
Intensive reading
A student should be able to:
·         Read a comprehension in proper pronunciation following all punctuations
·         Understand read work and translate it precisely 
A tutor should direct student in
·          Extensive reading, and reading for pleasure.
·         Story narrating and describing
·         Oral vocabulary and spelling drills
·         Intensive reading – for the required
·          











TH104 MAFUNDISHO YA KIKRISTO
Kosi itahusisha utafiti wa muungano wa kitheologia katika matumizi ya biblia kwamba umoja huo utasaidia katika utafasiri katika mfumo wa mafundisho ya Kibiblia. Kwamba tutachungua mwendelezo wa ufunuo wa Mungu kwa wanadamu kama ilivyo andikwa kwenye Biblia na kutafuta jinsi kila kipengele cha ufunuo huo kilivyo na uhusiano na matawi mengine ya theologia.

Mwisho wa Kosi mwanachuo atakuwa na uwezo wa:
·         Kufafanua maana na umuhimu wa Mafundisho ya Kibiblia
·         Kutengeneza mchoro wenye kuonyesha hatua za ufunuo wa Agano la Kale kama ufunuo wa ufalme wa Mungu
·         kuchambua dhima za Agano la Kale na kuzielezea jinsi zinavyoendelezwa katika kanuni na kutimilika katika Agano Jipya
·         Kuelezea mambo ya msingi ya kimafundisho katika Agano la Kale na jinsi yaligyo dhihilika katika kazi za Yesu Kristo
·         Kutumia njia ya kufundishia Mafundisho ya kibiblia na kuonyesha nafasi ya aya za Agano la Kale kwa wakristo wa leo.
·         Kuelewa mafundisho ya Paulo na kuyatumia katika maisha binafsi, jamii na kanisa kwa ujumla.

Mambo muhimu kwa mwanachuo kufanya katika kozi hii
Mwanachuo anatakiwa kuhudhuria na kushiriki katika jumla ya vipindi 270 kwa miaka yote mitatu.
Kila semester aandike insha mbili: moja binafsi na nyingine kwa makundi ambayo itawakilishwa kwenye semina kabla ya kukusanywa kwa mkufunzi.
Mwanachua atafanya majaribio yasiyopungua mawili kwa kila semester

MADA
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
TH104 Utangulizi wa Mafundisho Kikristo

1.    Maana ya Kitheologia

Mwanachuo aweze kuelewa:
1.    Kueleza maana na matumizi sahihi ya theologia ya Kikristo katika ulimwengu wa sasa.
2.    Kufafanua kanuni za maandiko Matakatifu.
Mkufunzi awaongoze wanachuo
1.      Kujadili na kueleza maana ya Theologia.
2.      Kujadili kanuni na chimbuko la Agano la Kale na Agano Jipya.
3.      Kujenga misingi ya ufasili wa Biblia

Je wanachuo wanaweza kueleza maana ya Mafundisho ya Kikristo?
15

b)      Historia na vitengo vya theologia

Mwanachuo aweze:
1.      Kueleza historia ya mafundisho ya Kikristo
2.      Kutaja na kueleza matawi ya theologia
3.      Kutumia uzoefu wake kuelezea maudhui ya kitheologia katika ulimwengu wa sasa
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.    Kujadili historia ya theologia
2.    Kutaja na kuelezea maana na matumizi ya vitengo vya theologia.
3.    Kuonisha vitengo vya theologian na hali ya kanisa leo.

 Je, wanachuo wanaweza kueleza historia na kutaja vitengo vya theologia?
15

c)      Mafundisho ya Kikristo juu ya uwepo wa Mungu na tabia zake


Mwanachuo aweze kueleza:
1.    Asili ya Mungu kutokana na uzoefu wake.
2.    Kueleza juu Mungu wa Kikristo
3.    Kutaja na kueleza sifa za Mungu na uwepo wake
4.    Kuchanganua changamoto za Kiafrika dhidi ya Mungu
Mkufunzi awaelekeze wanachuo
1.      Kujadili juu ya nafasi ya Mungu katika maisha yao.
2.      Kujadili mafundisho ya Kikristo juu ya Mungu
3.      Kufikiri na kupambanua ukweli wa kifalsafa za kiafrika juu ya uwepo wa Mungu

 Je, wanachuo wanaweza kutumia uzoefu wao katika kumwelezea Mungu na kukabiliana na changamoto mpya?
15

d)      Mafundisho juu ya Utawala wa Mungu



Mwanachuo awe na uwezo wa:
a)      Kuonyesha nafasi ya Mungu tangu uumbaji na mwendelezo wa utawala wake leo
b)      Kulinganisha na kutofautisha nafasi katika kuutunza ulimwengu dhidi ya majanga mbali mbali
c)      Kueleza dhana ya haki sawa kwa wote
d)      Kutumia nguvu za Mungu katika kukabiliana na nguvu za giza

Mkufunzi awaongoze wanachuo
1.    Kujadili uwezo na utawala wa Mungu
2.    Kutafakari juu ya nafasi ya Mwanadamu katika Uumbaji leo.
3.    Kuchambua falsafa mbalimbali juu ya nguvu za Mungu
4.    Kujadili na kupambanua malaika, mapepo, majini na jinsi ya kuweza kushirikiana ama kupingana nayo.


 Je, wanachuo wana weredi wa kutosha katika kutambua uwezo  wa Mungu na katika maisha yao na huduma yao?

TH204
 Mafundisho ya Kikristo juu ya Mazingira
a)      Utangulizi wa Mafundisho ya Kikristo juu ya Uumbaji
Mwanachuo awe na uwezo wa:
1.    Kueleza na kuchambua  mpango wa Mungu wa uumbaji
Mkufunzi awawezeshe wanachuo:
      1.     Kujadili maana na kuelezea juu ya mpango wa Mungu kwa viumbe vyake

Je, mwanachuo anashiriki kuboresha mazingira anamoishi na kuwa tabia endelezi?
Je, anatambua utunzaji wa mazingira ni wajibu na baraka za Mungu?
45

1.    Anguko na Mahusiano na Mazingira
Mwanachuo awe na uwezo:
1  Kueleza uhusiano kati ya kutii na baraka, laana na kutotii
2.    Kufafanua hali ya ardhi baada ya anguko na mahusiano ya mabadiliko ya hali ya hewa katika ulimwengu wa sasa.
3.    Kueleza matumizi ya teknolojia na athari zake katika mazingira
4.    Kutunza mazingira kama baraka za Mungu kwake.
 Mkufunzi awaongoze    wanachuo:
·         Kufanya ulinganifu wa kiumbaji
·         Kuchunguza athari ya kutotii na mchango wake ulimwenguni leo
·         Kusimamia majadiliano yahusuyo matumizi ya sayansi na teknolojia; faida na hasara zake
·         Kushiriki kwa vitendo kwenye utunzaji wa mazingira (kuanzisha vitaru vya miti, uteketezaji wa taka ngumu, urutibishaji wa ardhi kwa njia za asili).



5.    Dhana ya Kiafrika katika utunzaji wa maError! No table of contents entries found.zingira
Mwanachuo awe na uwezo:
1.    Kutofautisha mikazo ya kiafrika na ya Kikristo katika utunzaji wa mazingira
2.    Kutumia mbinu sahihi za kiafrika kwenye utunzaji wa mazingira.
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:
·         Kutafiti na kujadili hali ya mwafrika na mazingira
·         Kuchambua mbinu mbalimbali zinazotumika Afrika kupambana na hali ya uharibifu wa mazingira
·         Kuoanisha mbinu hizo na athari za mbinu za kisayansi katika kukabiliana uharibifu wa mazingira.


Mafundisho juu ya Utatu
a) Utangulizi wa mafundisho juu ya Utatu
Mwanachuo aweze kujadili na kueleza
1.    Maana na asili ya mafundisho ya utatu
2.    Falsafa mbali mbali juu ya utatu na utumikaji wake leo
3.    Thamani ya Utatu kwa kanisa la leo
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
·         Kujadili kwa mantiki maana na asili ya mafundisho juu ya UTATU
·         Kuwaelekeza falsafa sahihi juu ya Utatu hasa katika kipindi cha matengenezo ya kanisa
·         Kueleza umuhimu wa kujifuna UTATU katika kozi hii.


45

b) Mamlaka ya Utatu
Mwanachuo aweze:
1.    Kueleza nafasi ya Utatu katika historia ya imani na kwa kanisa leo.
2.    Kujadili na kupambanu kazi za Mungu baba, mwana na Roho Mtakatifu
3.    Kueleza uhusiano kati ya nafsi za Mungu
 Mkufunzi awawezeshe    
 wanachuo kujadili kwa  
 kina:
·         Mahusiano kati ya Nafsi Tatu za Mungu, kazi zao na mamlaka
 Baba – muumbaji
 Mwana – mkombozi
 Roho Mtakatifu –  
 Mtakasaji




c) Utatu na Kanisa
Mwanachuo aweze:
1.    Kwa vitendo, aeleza kazi wazi za Utatu katika kanisa.
2.    Kuongoza mdahalo uhusuyo Utatu Mtakatifu
3.    Kutetea mafundisho yahusuyo Utatu dhidi ya mitazamo potofu toka ndani na nje ya Ukristo
Mkufunzi ashirikiane na wanachuo:
·         Kutumia uzoefu kufanyike mjadala wa namna karama, miujiza, mafunuo nk zinavyoonekana wazi kwa kanisa leo.
·         Kuwajengea wanachuo uwezo wa kutetea mafundisho juu ya UTATU dhidi ya uzushi.



Mafundisho juu ya Utatu
a) Utangulizi wa mafundisho juu ya Utatu
Mwanachuo aweze kujadili na kueleza
4.    Maana na asili ya mafundisho ya utatu
5.    Falsafa mbali mbali juu ya utatu na utumikaji wake leo
6.    Thamani ya Utatu kwa kanisa la leo
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
·         Kujadili kwa mantiki maana na asili ya mafundisho juu ya UTATU
·         Kuwaelekeza falsafa sahihi juu ya Utatu hasa katika kipindi cha matengenezo ya kanisa
·         Kueleza umuhimu wa kujifuna UTATU katika kozi hii.


TH304 Mafundisho ya Kibiblia
·         Maana ya Mafundisho ya Kibiblia
Mwanachuo aweze:
·         Kueleza maana ya muunganiko wa mafundisho ya kibiblia.
·         Kutumia mfumo huo katika mahubiri.
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
·         Kulinganisha sehemu za Biblia katika mahubiri au mafundisho
·         Kufanya mzoezi kwa kusema na kuandika mfumo wa ufafanuzi wa kibiblia.


3

·         Muungano wa Mwanzo 1 – 11 na Ufunuo 20 – 22

Mwanachuo aweze:
·         Kuchambua na kueleza sehemu za biblia kwa muungano
·         Kuchungua dhamira zilizomo katika Mwanzo na Ufunuo.
·         Kutumia Biblia kueleza vifungu tangulizi.

Mkufunzi awaongoze wanachuo:
·         Kusoma na kuchungua dhamira zilizomo kati ya Mwanzo na Ufunuo wa Yohana
·         Kumwandaa mwanachuo kutaali Biblia akifafanua maandiko


7

a)      Kuchanganua dhamira za kibiblia kama vile:
  1. Uumbaji
  2. Ardhi
  3. Neema
  4. Sheria
  5. Baraka
  6. Dhambi
  7. Hofu
  8. Hukumu
  9. Ufalme wa Mungu
  10. Rushwa
  11. Wokovu
  12. Upatanisho
  13. Mungu kufanyika mwanadamu
  14. Kifo
  15. Ufufuo
  16. Msalaba
  17. Laana
  18. Familia
  19. Mazingira
  20. Masikini
Mwanachuo aweze:
1.    Kuchagua dhamira kuu za kuzijadili na kuzitolea andiko.
2.    Kueleza hadharani dhamira hizo kwa notisi au bila notisi.
3.    Kuonyesha dhima hizo  jinsi zinavyofaa katika mazingira ya sasa.
4.    Kuchagua dhamira yoyote aipendayo na kuchambua katika mfumo wa mafundisho ya kibiblia
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
·         Kutumia mfumo waliojifunza katika kufanya uchambuzi wa moja ya dhamira watakayopewa.
·         Kusimamia na kuhakiki kazi mradi ya wanachuo.



35
Mafundisho ya Paulo

a)      Utangulizi wa Theologia ya Paulo
      1.     Maisha ya Sauli Kabla ya kuongoka
      2.     Kuanzia barabarani kwenda Dameski

Mwanachuo aweze:
·         Kueleza na kufafanua maisha ya Sauli kabla hadi barabarani kwenda Dameski.
·         Kuchambua uzoefu wa awali wa Sauli katika maswala ya imani
Mkufunzi awaelekeze wanachuo kujadili:
·         Kueleza historia ya maisha ya Paulo kabla ya kuokolewa.
·         Kujadili kwa kina muujiza uliobadili hali ya Sauli
·         Kutumia historia ya awali ya Sauli katika kuchambua huduma na mafundisho yake



16


b)      Mafundisho yake katika Nyaraka juu ya Mungu: Baba, Kristo na Roho Mtakatifu, Wokovu, Upatanisho, dhambi, mauti, kutakatifunzwa, ufufuo, mwanamke, uongozi wa kanisa, utawala wa kiserikali na kanisa nk.





Mwanachuo atakuwa na uwezo wa:
·         Kutaja na kueleza dhamira za nyaraka
·         Kuchambua mafundisho ya Paulo kwa kulinganisha na tukio la njiani kwenda Dameski
·         Kutumia historia yake ya Kiyahudi katika ufafanuzi wa mafundisho ya Paulo
·         Kueleza kwa ufasaha na umahili wote changamoto zilizomo katika mfundisho ya Paulo leo
·         Kutumia nafasi ya Paulo kuchochea karama ya Uinjilisti katika dayosisi yake/huduma yake.
·         Kutumia makundi mbalimbali yaliyomo kanisani ili kuujenga mwili wa Kristo. Kama vile: UMAKI, Vijana, Wazee, na watoto.
·         Kutumia maarifa ya stadi za kazi alizojifunza ili kukidhi haja ya gharama za kiutumishi na familia yake.
Mkufunzi ahakikishe wanachuo:
Wanachuo wanajadili dhamira katika mafundisho ya Paulo na kuzielewa na kulinganisha jinsi mafundisho hayo yanavyoweza kufundishwa leo



Mkufunzi awape nafasi wanachuo kutumia:
·         Uzoefu wao wa wokovu na huduma, ili kujadili changamoto za Paulo kwa  vitendo na kwa uhalisia.
·         Kuandaa mpango wa uinjilisti na kuutekeleza kwa vitendo




29















TH103 AGANO LA KALE
Lengo kuu la Kozi ya Agano la Kale kwa miaka mitatu:
Kosi itamsaidia mwanachuo kujifunza maudhui , historia na lugha iliyotumika kwenye  Agano la Kale na umuhimu wake kwa kanisa la leo.
Mwisho wa kosi mwanchuo atakuwa anao uwezo wa;
·         Kuelezea na kuchanganua historia ya uwepo wa Agano la Kale na Kanuni za maandiko hayo na mwendelezo mzima wa historia hiyo.
·         Kufanya mhutasari wa Agano la kale kulingana na vitabu vitakavyotumika
·         Kuoanisha Agano la Kale kama mwanzo wa mpango wa Mungu wa wokovu na kutimilika katika Agano Jipya.
·         Kumwelezea Yesu katika Agano la Kale
·         Kutumia Agano la Kale kama msingi wa mahubiri

Mambo muhimu kwa mwanachuo kufanya katika kozi hii
Mwanachuo anatakiwa kuhudhuria na kushiriki katika jumla ya vipindi 270 kwa miaka yote mitatu. Kila semester mwanachuo anatakiwa kukamilisha vipindi 45
Kila semester aandike insha mbili: moja binafsi na nyingine kwa makundi ambayo itawakilishwa kwenye semina kabla ya kukusanywa kwa mkufunzi.
Mwanachuo atafanya majaribio yasiyopungua mawili kwa kila semester
Mwanachuo ataendelea na kozi nyingine baada ya kufaulu vyema kozi tangulizi kwa zaidi ya 50% ya kazi zote za darasa

MADA
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
TH105: Utangulizi wa Agano la Kale:
a)      Historia ya Palestina wakati wa Agano la Kale
Mwanachuo aweze;
3.      Kuchora ramani ya palestina na kuonyesha maeneo muhimu
4.      Kutaja na kueleza wasifu wa wahusika wakuu katika historia
5.      Kutaja dola za wakati wa Agano la kale
6.      Kanuni za AK
Mkufunzu awaongoze wanachuo:
1.      Kuchora na kutaja kwa usahihi maeneo maalum ya kihistoria katika Palestina wakati wa AK
2.      Kujadili wahusika wakuu katika zama hizo
3.      Kuchunguza dola na mchango wao katika kupatikana kwa AK
4.      Kujadili kwa kutaja sababu za kanuni za AK na vitabu vya Apokrifa

Je wanachuo wanaweza kueleza maana na historia ya AK na
10

b) Dhamira za uumbaji
Mwanachuo aweze:
1        Kujadili Mwanzo 1-3  na kupambanua kazi za uumbaji
2        Kulinganisha uumbaji wa kibiblia na hadithi zingine zihusuzo Uumbaji hasa Mashariki ya Kati na Afrika
3        Kutetea hoja ya undelevu wa uumbaji
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1        Kujua maana ya uumbaji  wa Kibiblia na kutofautisha na hadithi zingine
2        Kutambua kuwa Mungu ndiye mwenye kuumba vitu vyote: vionekanavyo na visivyoonekana.
Je, wanachuo wanao ujuvi wa kuelezea bayana uumbaji wa Mungu?

35

a) Ufalme wa Mungu

Mkufunzu awaongoze wanachuo:
1.      Kujadili na kusoma vitabu na majalida yahusuyo Ufalme wa Mungu.
2.      Kufahamu sifa za Ufalme wa Mungu na muundo wa utawala wa kimungu
3.      Kulinganisha kuwepo na kutokuwepo kwa Utawala wa Mungu miongoni mwa watu wake
4.      Kufikia kilele cha ahadi za Mungu za kurudi tena miongoni mwao

Je wanachuo wanaweza kupambanua maana na mamlaka ya Mungu mbele ya ulimwengu?

Je, wanachuo wanaamini kwamba ufalme wa Mungu upo na bado, utakamilishwa arudipo Yesu?
25

b)      Uchambuzi wa Vitabu vya Pentatuki.

Mwanachuo  aweze:
1.      Kuchunguza na kueleza:
·         Jina la kitabu,
·         Mwandishi ,
·         Tarehe ya uandishi,
·         kusudi/lengo,
·         Mtindo na fasihi yake
·         Wahusika wakuu,
·         Mafundisho yaliyomo
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kujadili mpango wa uandishi wa vitabu vya Sheria
2.      Kutaja mwandishi, tarehe ya uandishi, mtindo , wahusika wakuu na mafundisho yaliyomo.


Je, mwanachuo ameweza kujadili na kuelezea vitabu vya Pentantuk na Yoshua?

20
TH205 UCHAMBUZI WA VITABU VYA PENTATUKI NA MANABII WADOGO
Mwanzo 12-45
Mwanachuo aweze:
2.      Kueleza mpango wa Mungu kwa Taifa na watu wake.
3.      Ahadi za Mungu
4.      Maagano ya Mungu
5.      Baraka na utiii
6.      Kutotii ni laana
7.      Mababa wa Imani
8.      Kutengeneza Taifa la Israeli
9.      Utumwani Misri nk.
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kusoma sura zote za Kitabu cha Mwanzo 12 hadi mwisho
2.      Kujadili na kuelewa mafundisho, matukio kwa jinsi yalivyotukia kihistoria.
3.      Kuchambua mafundisho yapatikanayo ndani ya sura husika.



15

Kitabu cha Kutoka
Mwachuo aweze:
1.      Kueleza picha kubwa ya Kitabu cha Kutoka kwa kulinganisha na Kitabu cha Mwanzo.
2.      Kueleza maisa ya Israel kabla ya sura  13
3.      Kueleza mafundisho muhimu yapatikanayo katika Kitabu cha Kutoka:
·         Mungu Mfalme
·         Utumwa
·         Wito
·         Miujiza na ishara
·         Upinzani kwa kazi ya Mungu
·         Ukombozi
·         Pasaka
·         Sheria .
Uongozi shirikishi
Mkufunzi awaongoze wanachuo

1.      Kusoma angalau sura zisizopungua 3 kwa kila siku.
2.      Kufanya utafiti juu ya kitabu cha Kutoka kwa kuchunguza mwanzo wake kama mwendelezo wa Kitabu cha Mwanzo
3.      Kutaja na kuchambua kwa ufasaha mafundisho yote yaliyomo kitabuni.
4.      Kuibua changamoto zinazo hitaji majibu kaitka maisha ya leo


Je, wanachuo wanaweza kuhubiri na kutoa maelezo juu ya mafundisho ya vitabu hivi?

15

Kitabu cha Kumbukumbu la Torati, Mambo ya Walawi na Joshua.
Mwanachuo aweze:
1.      Kusoma na Kuchambua vitabu vyote kwa kueleza dhamira kuu zilizomo
2.      Kujadili na kuelewa zaidi katika:
·         Sheria ya ukuhani
·         Utakaso na kutakaswa
·         Sheria za Musa
·         Agano la Mungu
·         Uongozi
·         Sheria ya ardhi nk.
·         Kumtumikia Mungu

Mkufunzi amwongoze mwanachuo:
1.      Kujadili katika vikundi na kusoma vitabu na vitini juu ya mada hii
2.      Kuchambua dhima zilizomo na kuandika ufupisho wa dhima hizo
3.      Kulinganisha vitabu hiyo na Waraka kwa warumi na Waebrania
4.      Kutumia mafundisho kuweka msingi wa maisha ya kanisa leo.

Je, wanachuo wanatumia dhima za vitabu hivi katika maisha yao ya kila siku?


Je, wanachuo wanaweza kuchanganua, kulinganisha na kutofautisha sheria na neema katika kuhesabiwa haki?






15
Uchambuzi wa Vitabu vya manabii
a)      Utamgulizi wa Vitabu vya Manabii:
Wa mwanzo
Mwanachuo aweze:
1.      Kuchambua baadhi ya vitabu vya manabii wa mwanzo hasa Nehemia, Daniel, Ezekieli
Mkufunzu awaongoze wanachuo:
1.      Kuelewa mazingira ya manabii wa mwanzo.
2.      Kuawinisha ujumbe wa manabii hao na hali halisi ya maisha katika ulimwengu wetu leo.

Je wanachuo wanaweza kueleza kazi na ujumbe wa Manabii wa kale?
45
TH305: UCHAMBUZI KITABU CHA WIMBO ULIO BORA NA MITHALI
a)      Kitabu cha Mithali
Mwanachuo aweze:
1.      Kutaja na kuelezea juu ya Uandishi, mtindo na  tarehe.
2.      Kufanya uchambuzi wa mafundisho muhimu yapatikanayo katika kitabu cha Methali.
Mkufunzu awaongoze wanachuo:
1.      Kutafiti kwa kusoma utangulizi wa Kitabu cha Mithali
2.      Kusoma sura zote za kitabu hicho.
3.      Kujadili mafundisho yaliyomo kwenye kitabu hicho.

Je wanachuo wanaweza kueleza kazi na ujumbe wa Manabii wa kale?
15

b)      Kitabu cha Wimbo Ulio Bora
Mwanachuo aweze:
1.      Kuelewa kusudi la Kitabu hiki kuingizwa katika Biblia (Kanuni ya Kimaandiko)
2.      Kumpa Yesu nafasi katika maelezo ya Kitabu hiki.
3.      Kuelezea uhalisia wa Kitabu hiki na maisha ya kawaida ya ndoa na jamii.
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kusoma kitabu hiki na kutafakari sura zote.
2.      Kujadili uandishi, na mafundisho yaliyomo
3.      Kutumia kitabu hiki katika mahubiri ya kiinjili.

Je, mwanachuo ameweza kusoma, kuelewa lengo la uandishi wa kitabu cha Wimbo Ulio Bora?

Je, mwanachuo anaweza kumwonyesha Yesu kama kiini cha mafundisho ya kitabu cha Wimbo Ulio Bora.
15
UCHAMBUZI WA VITABU VYA MANABII WA KALE, ZABURI NA AYUBU
a)      Kitabu cha Nabii Isaya
Mwanachuo aweze:
1.      Kuelezea historia ya Nabii Isaya na maisha yake ya unabii.
2.      Kueleza changamoto alizokutana nazo kama nabii
3.      Kujadili matuini ya masihi na utabiri wa kuzaliwa kwa Yesu, maisha yake na kusudi la kuja kwake duniani.
4.      Kutumia mafundisho mengine ya unabii wa kitabu hiki katika kutafakari maisha yetu mbele za Mungu.
Mkufunzu awaongoze wanachuo:
1.      Kueleza umuhimu wa Unabii wa kitabu cha Nabii Isaya; enzi zake na wakati huu
2.      Kujadili na kuelewa mafundisho ya msingi ya Unabii wa kitabu cha Isaya: Utakaso wa dhambi, Masiha, Ukombozi, Mateso ya Masiha, wito, nk.
3.      Kutumia mafundisho ya unabii wa kitabu cha Nabii Isaya katika huduma na maisha ya kila siku

Je, wanachuo wanaweza kuchambua Unabii wa kitabu hiki na kutumia unabii huo katika kukuwa kiimani?
15

b)      Kitabu cha Nabii Yeremia
Mwanachuo aweze:
1.      Kujadili na kueleza lugha za picha kama zinavyotumika katika unabii wa kitabu hiki.
2.      Kufafanua mafundisho yaliyomo katika kitabu hiki. Km. Unabii wa Agano Jipya, Kukombolewa, (Mambo yajayo)
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kufanya utafiti juu ya Kitabu cha Nabii Yeremia
2.      Kufahamu mafundisho yake
3.      Kueleza umuhimu wa mafundisho hayo kwa kanisa la leo

Je, wanachuo wanaweza kuchambua Unabii wa kitabu hiki na kutumia unabii huo katika kukuwa kiimani?
15

a)      Uchambuzi wa Kitabu cha Zaburi.
Mwanachuo aweze:
1.      Kuchambua na kueleza aina zote za Zaburi na waandishi wake.
2.      Kuelezea maana na umuhimu wa Zaburi kwa wasomaji wa kwanza
3.      Kutumia mafundisho ya Zaburi kama msingi wa mafundisho ya Kikristo leo.
Mkufunzu awaongoze wanachuo:
1.      Kujadili na kufafanua sehemu na muundo wa Zaburi.
2.      Kutaali kitabu cha Zaburi kwa kulinganisha na sehemu zote za Biblia.
3.      Kufanya maandalizi ya mahubiri na kuhubiri kwa kutumia Zaburi.
4.      Kutengeneza Zaburi binafsi yenye kuaksi maisha yake

Je, wanachuo wanaweza kutumia mafundisho ya Zaburi katika kuhubiri?

Je, wanachuo wanaweza kutumia muundo wa Zaburi kutengeneza zaburi zingine kutokana na uzoefu wao?
15

b)     Uchambuzi wa Kitabu cha Ayubu
Mwanachuo aweze:
1.      Kufahamu mazingira ya Kitabu cha Ayubu: Jiografia, uandishi, na mafundisho
2.      Kujadili mafundisho ya kitabu hiki.
3.      Kuelewa na kuelezea bayana dhima mbalimbali za kitabu hiki km. Uadilifu na ukamilifu, Baraka za Mungu, majaribu nk.
4.      Kutumia kitabu hiki kueleza ukweli kuhusu maisha ya mkristo katika kuitetea imani yake
Mkufunzi anatakiwa kuwaongoza wanachuo:
1.      Kuchungua kitaaluma mazingira ya kitabu cha Ayubu
2.      Kusimamia mijadala ya kiutafiti juu ya mafundisho ya kitabu cha Ayubu.
3.      Kutambulisha maisha ya Ayubu kuwa sehemu ya mapito ya maisha ya muhudu na yenye kuimarisha imani
4.      Kutambua Baraka za Mungu hupatikana baada ya kupita katika majaribu.

Je, mwanachuo anaweza kuhimili majaribu yampatayo na kuyahimili?

Je, hutumia njia zipi kuwatambulisha wakristo kutambua na kusimamia majaribu yao?
15










                       

















TH101 AGANO JIPYA
Lengo kuu la Kozi ya Agano Jipya kwa miaka mitatu:
Mwisho wa kozi hii mwanachuo atakuwa na uwezo wa;
·         Kuelezea mazingira ya Agano Jipya kabla na baada ya Kristo
·         Kuonyesha uwezo wa kimaarifa juu ya fasihi ya Agano Jipya, zikiwemo: muundo, dhima, lengo na yaliyomo.
·         Kutofautisha na kulinganisha Injili nne
·         Kueleza na kuhubiri Nyaraka na Injili kitheologia na kiinjili ili kukidhi hitaji la wakristo wa sasa.
·         Kutambua na kueleza tofauti mbalimbali za mafafanuzi ya Injili (Gospel’s criticism)

Mambo muhimu kwa mwanachuo kufanya katika kozi hii
Mwanachuo anatakiwa kuhudhuria na kushiriki katika jumla ya vipindi 270 kwa miaka yote mitatu. Kila semester mwanachuo anatakiwa kukamilisha vipindi 45
Kila semester aandike insha mbili: moja binafsi na nyingine kwa makundi ambayo itawakilishwa kwenye semina kabla ya kukusanywa kwa mkufunzi.
Mwanachua atafanya majaribio yasiyopungua mawili kwa kila semester

MADA
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
TH101: UTANGULIZI WA AGANO LA JIPYA

b)    Utangulizi wa Agano Jipya
Mwanachuo aweze kuelewa;
5.    Maana ya Agano Jipya
6.    Kufahamu vyanzo, mgawanyiko na vitabu vya AJ
7.    Kuelewa jinsi Agano la Kale lilivyoendelezwa katika Agano Jipya
8.    Agano jipya kabla, wakati, na baada ya Kristo.
9.    Kueleza historia ya Palestina tangu Babeli wakati wa mfalme Nebukadineza hadi wakati wa Kristo
Mkufunzi awaongoze wanachuo
4.    Kusoma vitabu mbalimbali vya Agano Jipya,
5.    Kugawa Agano Jipya katika makundi husika.
6.    Kutaali Agano Jipya katika kipindi endelevu.


Je wanachuo wameweza kuelewa kwa kiwango cha kuelezea mazingira ya Agano Jipya kabla na baada ya Kristo?

Wameweza kuonyesha uwezo wa kimaarifa juu ya fasihi ya Agano Jipya, zikiwemo muundo, dhima, na mgawanyiko wake.
45
 b) Utangulizi AJ; Injili ya Marko, Luka, Mathayo na Yohana
Mwanachuo aweze;
3.    Kuelewa hatua za uchambuzi wa vitabu vya Injili na aweze kuvitumia ipasavyo.
4.    Kuelewa mfananano na tofauti uliopo kati ya vitabu vya Injili.
5.    Uchambuzi wa kina wa Injili ya Yohana
Mkufunzi awaongoze wanachuo
5.    Kufanya uchambuzi katika vitabu vya Injili ya Marko Luka na Mathayo.
6.    Kuchambua mfanano kati ya Injili tatu (Marko, Luka, Mathayo)
7.    Kuchambua, kujadili, na kuweka katika vitendo mafundisho ya Injili ya Yohana.

Je, wanachuo wameelewa chimbuko, mgawanyiko na mfanano katika Injili tulizonazo katika Biblia?

Je wameweza kuwa mahiri katika kutumia mafundisho ya Injili katika huduma yao ya kila siku?
45
TH201:
UFAFANUZI WA MATENDO YA MITUME NA WAEBRANIA 







c)  Kitabu cha Matendo ya mitume


Mwanachuo aweze kuelewa:
6.    Kitabu cha historia katika Agano Jipya.
7.    Kuelewa jinsi kanisa lilivyozaliwa.
8.    Kuelewa Pentecosti na theologia yake katika kanisa la mitume.
9.    kujifunza na kuelewa misingi ya utume na uinjilisti
10.              Maisha ya kikristo baada ya kuzaliwa mara ya pili.
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:
4.    Kusoma na kujadili misingi ya kanisa kwa mtazamo wa kitabu cha matendo ya mitume.
5.    Kulinganisha mbinu za kiutume wakati wa mitume, baada na wakati wa sasa.
6.    Changamoto ya kupanda makanisa katika ulimwengu wa sasa.
7.    Uhusiano wa kitabu cha Matendo ya Mitume na nyaraka za Paulo.


Je, wanachuo wana uweredi wa kutosha katika kutafiti mbinu sahii za ki-Uinjilisti?

Je wameweza kujadili na kuweka katika vitendo mafundisho makuu ya kitabu cha Matendo ya Mitume?
45
d) Agano la Kale katika Agano Jipya (kitabu cha Waebrania)





Mwanachuo aweze:
5.    Kuelewa maana ya Agano la Mungu na wanadamu
6.    kuelewa na kutafiti wakati wa ukimya
7.    Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu katika Agano zote mbili
8.    Historia ya watu wa Mungu na safari ya wana wa ahadi
9.    Taifa la watu wa Mungu na historia yao
10.              Ukuhani wa Agano la Kale na Jipya
11.              Ukuhani wa Yesu katika kitabu cha Waebrania
ovuti na faida zake.
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:
2.    Kujadili na kueleza maana ya Agano katika wakati unaoendelea.
3.    Kuchambua mahusiano baina ya Agano la Kale na Jipya
4.    Kutafiti historia ya ulimwengu wa Kikristo
5.    Kuchambua utata wa Injili mfanano (Synoptic problems)
6.    Kumtafuta na kumuona Yesu katika Agano la Kale
7.    Kuona utegemezi uliopo kati ya AJ na AK
8.    Kutofautisha ukuhani wa AK na ule wa Yesu Kristo katika Waebrania.



Je, wanachuo wanaweza kutumia ipasavyo maandiko ya AK na AJ katika huduma yao hasa katika Mahubiri?

Je, wanachuo wanaweza kumwelezea Yesu katika Agano la Kale?

Je wanaweza kutofautisha Ukuhani na Uchungaji?
45
TH301 UFAFANUZI WA WARAKA KWA WARUMI NA UFUNUO WA YOHANA 
(e) Waraka kwa Warumi



















Mwanachuo aweze kuelewa:-
1.      Utangulizi na mwandishi wa waraka huu.
2.      Mazingira ya Mji wa Rumi na jinsi kanisa lilivyozaliwa huko.
3.      Mafundisho makuu katika waraka huu
4.      Msalaba, Upataniso, Haki, Rehema, Kanisa, nk.
5.      Nafasi na mchango wa waraka huu katika kukua kiroho
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:-

1.      Kusoma na kuchambua kwa makini mafafanuzi ya waraka kwa Warumi.
2.      Kuweka katika vitendo mafundisho makuu ya waraka huu.
3.      Changamoto zinazoikumba kanisa la leo dhidi ya mafundisho makuu ya waraka huu



Je wanachuo wanaweza kufundisha kwa ufasaha kitabu hiki katika mafundisho, mahubiri na kuishi kwa mfano wa Paulo?
45
(f) Ufunuo wa Yohana
Mwanachuo aweze kuelewa:-
1.      Mwandishi, Utangulizi na mazingira ya kitabu hiki.
2.      Kuchambua kwa kina asili ya maandiko ya kimafunuo, lengo na makusudi  yake.
3.      Lugha na matumizi ya Ishara katika waraka huu
4.      Dhana ya wakati kwa mtazamo wa Ufunuo
5.      Uhusiano na umuhimu wa waraka huu katika maisha ya kila siku ya kanisa.
Mkufunzi awaongoze wanachuo:-
1.      Kusoma mafafanuzi ya kitabu cha Ufunuo
2.      Kuangalia uwiano wa matukio yanayoripotiwa katika kitabu hiki na historia ya matukio mengine katika ulimwengu wa kikristo.
3.      Kutumia mifano na ishara za wakati wa sasa katika kufafanua mifano na ishara katika kitabu cha Ufunuo
4.      Kuwianisha na kuhusianisha ufunuo na vitabu vingine vya mafunuo katika Biblia.
5.      Jinsi ya kutumia kitabu cha Ufunuo katika maisha ya kila siku.

Je wanachuo wameweza kuelewa mazingira, lengo na jinsi ya kutumia kitabu cha ufunuo katika huduma ya kanisa?
Je wameweza kufafanua kitabu hiki kwa kuifundisha na kuihubiri kwa ufasaha?
Je wameelewa jinsi ya kutumia kitabu hiki katika kuhudumia kanisa na jamii kwa ujumla?
45






PT103 UCHUNGAJI
Kosi hii imeandaliwa ili kumfanya mwanachuo kutambua huduma ya kichungaji na kukubaliana na changamoto za maisha ya ulimwengu wa sasa ili kumwandalia Kristo wateule, vile vile kuelewa mafundisho mbalimbali yahusuyo huduma ya kichungaji kama utawala, falsafa za kichungaji, n.k
Mwisho wa kozi mwanachuo atakuwa na uwezo wa:
·         Kujitambua na kutenda kichungaji kwa kuishi maisha ya unyenyekevu mbele za Mungu na watu pia. Hatakuwa mwenye tabia ya kunung’unika bali atakuwa mbele siku zote kutatua na kushauri wenye mazoea ya kunung’unikia wengine.
·         Kuelezea uchungaji wa kibiblia na kutenda sawa sawa na kusudi la Mungu kwa daraja hili
·         Kuwa msimamizi na mwajibikaji kwa familia yake na kanisa la leo
·         Kuwa mwalimu, mshauri na kiongozi bora anayeongoza kanisa lake na familia yake.
·         Kutumia saikologia ya kichungaji katika kutatua matatizo binafsi na ya watu wanaomzunguka
·         Kuweza kukagua vitabu vya fedha, kupokea na kuchambua taarifa mbalimbali
·         Kuwa meneja mwenye ubunifu na mwenye kusimamia uchumi wa kanisa lake na familia yake mwenyewe
·         Kuwa kiongozi mwenye mamlaka katika eneo lake


Mambo muhimu kwa mwanachuo kufanya katika kozi hii
Mwanachuo anatakiwa kuhudhuria na kushiriki katika jumla ya vipindi 270 kwa miaka yote mitatu. Kila semester mwanachuo anatakiwa kukamilisha vipindi 45
Kila semester aandike insha mbili: moja binafsi na nyingine kwa makundi ambayo itawakilishwa kwenye semina kabla ya kukusanywa kwa mkufunzi.
Mwanachua atafanya majaribio yasiyopungua mawili kwa kila semester

MADA
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
PT103

MCHUNGAJI NA MHUBIRI
c)      Maana ya Uchungaji
Mwanachuo aweze:
3.      Kueleza kwa kufafanua maana ya Uchungaji na Mchungaji

Kujadili wajibu wa mchungaji
4.      Mchungaji ni mshauri
5.      Mchungaji ni mhudumu
6.      Mchungaji ni mwalimu
7.      Mchungaji ni mwombaji
8.      Mchungaji ni mwanajamii
9.      Mchungani ni mtawala
10.  Mchungaji ni kiongozi.
11.  Mchungaji ni mhubiri
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kujadili na kuelewa maana ya neno Mchungaji
2.      Kutaja na kujadili wajibu na sifa za mchungaji mahili.


Je, wanachuo wanaweza kueleza maana ya uchungaji na wajibu wake?


Je, wanachuo wanajitambua kama wachungaji na wanaonekana kubeba wajibu wa kichungaji?
45

d)      Mahubiri
Mwanachuo aweze:
1.      Kuelewa maana ya Mahubiri na umuhimu wake leo.
2.      Kufahamu na kueleza historia ya ufafanuzi wa Biblia na aina zake.
3.      Kutumia mbinu za mahubiri kuandaa na kuwasilisha kwa maandishi na bila maandishi kwa hadhira kubwa.
4.      Kuhubiri kwa namna ya kujihubiri mwenyewe ili kuokolewa na kutakaswa kwanza kabla ya hadhira.
5.      Kuhubiri kwa kutumia Utaratibu wa Masomo ili kuwapitisha wakristo katika Biblia na majira yote ya kanisa kwa mwaka mzima.




Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kujadili na kueleza maana ya Mahubiri na aina zake.
2.      Kutaja na kuelewa umuhimu wa mahubiri katika kanisa la leo
3.      Kutafiti historia ya ufafanuzi wa mahubiri na aina zake na kuchagua njia ifaayo kufafanulia Maandiko Matakatifu
4.      Kuhubiri hadharani, kanisani na nyumbani ili wasikiao wamwone Kristo kupitia sauti ya Mhubiri.
5.      Kuwafanya mazoezi ya kutosha ya kuhubiri: kwa muda mfupi sana (dakika 5-10) muda mrefu (dakika 30 – saa 1).
6.      Kujihubiri mwenyewe: Maisha yake yafanane na maneno yake na kuacha mazoea ya kushambulia.

Je, mwanachuo anaouwezo kueleza maana maana na asili ya mahubiri?


Je, mwanachuo anao uweredi wakutosha katika kufafanua kifungu cha maandiko na kuoanisha na vifungu vingine ili kuleta katika mazingira ya sasa ya hadhira yake?


PT113 FAMILIA YA KIKRISTO
a)      Utangulizi wa familia ya Mungu.
·         Maana ya familia ya Kikristo
·         Misingi ya familia ya Kikristo
·         Nafasi ya Familia katika mpango wa Mungu.

Mwanachuo aweze;
1.      Kuelewa misingi ya familia ya Kikristo
2.      Kufanya utafiti wa kibiblia na kubaini lengo na mpango wa Mungu juu ya familia.
3.      Kutumia familia kuu( Adamu, Ibrahimu, Yakobo, Daudi, Hezekia, Yusufu, Yesu, Paulo, kanisa, nk.) katika kuaksi familia za ulimwengu wa sasa.
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kujadili na kueleza maana ya familia na misingi yake kibiblia
2.      Kutafiti makusudi ya Mungu kuunda taasisi ya familia.
3.      Kutambua mtu mmoja kama familia (waseja).
4.      Kutumia familia tangulizi katika kuweka msingi wa familia ya sasa

Je, mwanachuo ameelewa vya kutosha umuhimu wa familia na kuwajibika katika familia yake?

Je, mwanachuo anatambua kuwa kanisa ni familia takatifu na hivyo anao wajibu mkuu kushiriki kama baba kwa familia yake?
45

b)      Ndoa
·         Ndoa za Kikristo
·         Ndoa za jadi
·         Kiserikali
·         Ndoa za dini mbalimbali
Mwanachuo aweze:
1.      Kueleza maana ya ndoa: kikanisa, kijadi, kisheria
2.      Kutofautisha kati ya ndoa ya kanisa, serikali, jadi na dini zingine.
3.      Kutambua nafasi ya mchungaji katika ndoa zote: Serikali, jadi na kikristo
4.      Kuandaa mafunzo yahusuyo uchumba hadi ndoa
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
1.      Kutoa maana mbali mbali ya neno Ndoa:
2.      Kujadili mitazamo mbali mbali juu ya ndoa: Ndoa ya mke mmoja au wengi, ndoa ya Kikristo, Dini zingine, serikali na jadi.
3.      Kujadili wajibu wa mchungaji kama wakala wa usajili wa ndoa.
4.      Kutengeneza mtaala wa kudumu wa mafunzo ya ndoa.
5.      Kufanya mazoezi ya kufundisha na kufungisha ndoa

Je, mwanachuo anaweza kuongoza darasa la kabla na baada ya ndoa?

PT203
SAIKOLOGIA YA KICHUNGAJI
a)      Utangulizi wa Saikologia ya Kichungaji
Mwanachuo aweze:
1.      Kuelewa na kutoa maana ya Saikolojia.
2.      Kujadili matawi mbalimbali ya Saikolojia
3.      Kujadilli maana na umuhimu kosi ya saikolojia ya Kichungaji na mtumizi yake

Mkufunzu awaongoze wanachuo:
1.      Kujadili Saikolojia na matawi yake.
2.      Kuongoza mjadala juu ya Saikolojia ya kichungaji: maana, umuhimu wake.
3.      kujadili uhusiano wa Saikolojia ya Kichungaji na aina zingine za Saikolojia.



Je, wanachuo wanaweza kueleza maana ya uchungaji na wajibu wa mchungaji?

45

b)      Saikolojia na falsafa yake (Wanasaikolojia)



c)      Saikolojia ya Makuzi

Mwanachuo aweze:
1.      Kuelezea hoja za mabingwa mbalimbali wa kisaikolojia wanaojadili makuzi ya mwanadamu.
2.      Kuelewa mitazamo ya ukuaji wa akili na mabadiliko tabia ya mwanadamu
3.      Kuelewa namna ya kusaidia makundi mbalimbali katika eneo husika.
Mkufunzi awasaidie wanachuo:
·        Kuchungua kwa usahihi asili ya saikolojia na matumizi yake.
·        Kuelezea hatua mbalimbali za ukuaji kiakili na athari zake katika uendeshaji wa shughuli za kanisa.




d)      Saikolojia katika mtazamo wa Kibiblia
Mwanachuo aweze:
1.      Kuonisha falsafa za makuzi  na mitazamo ya Kibiblia katika kushirikiana na makundi mbalimbali ya kijamii.
2.      Kutibu na kutatua matatizo ya msongo wa mawazo kwa njia za kisaikolojia na sala.
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
·        Kuisoma Biblia na kubainisha hali ya kisaikoljia ilivyotumika kutatua matatizo ya kijamii.
·        Kumtumia Yesu na Paulo kama wanasaikolojia wakuu wa zama zote katika kujifunza saikolojia ya Kibiblia.




e)      Saikolojia na Maadili ya kanisa
Mwanachuo aweze:
1.      Kueleza maana ya maadili
2.      Kuchambua wanafalsafa wa maadili na mitazamo yao.
3.      Kuoanisha falsafa hizo na mafundisho ya maadili ya Kikristo.
4.      Kutaja mambo muhimu yakuzingatiwa katika maadili ya kanisa la leo (Kitabu cha Mapasta)

Mkufunzi aonyeshe
·        Uhusiano uliopo kati ya Saikolojia na maadili ya kanisa
·        Kueleza maana ya maadili ya Kikristo
·        Kuelezea wataalam mbalimbali wa Maadili na changamoto zao




Je, mwanachuo anajimbua kwa uwezo na udhaifu wake, na anatumia vipi vyote viwili kutumikia kanisa la Mungu?

Je, mwanachuo anaouwezo kiasi gani kuvumilia na kukabiliana na changamoto tata toka kwa wanachuo wenzake?

PT213 USHAURI NASIHI WA KICHUNGAJI
Utangulizi wa Ushauri Nasihi wa Kichungaji
Mwanachuo aweze:
1.      Kuelewa na kutoa maana ya Ushauri wa Kichungaji.
2.      Kujadili sifa za mshauri bora
3.      Kujadili na kuelewa hatua mbalimbali za ushauri.
4.      Kutumia njia sahihi za Kibiblia katika kusaidia kuelewa na kufanya ushauri.

Mkufunzu awaongoze wanachuo:
4.      Kujadili Ushauri na matawi yake.
5.      Kuongoza mjadala juu ya ushauri wa kichungaji: maana, umuhimu wake.



Je, mwanachuo anao uweredi wa kutosha kufafanua, kutambua na kuongoza ushauri kwa makundi mbalimbali?
45

a)      Mshauri na Mteja:
Mwanachuo aweze:
1.      Kuelewa aina za wateja na namna ya kusaidiana nao katika kufikia suluhu.
2.      Kuunda mazingira yapasayo.
3.      Kutengeneza mazingira yapasayo kufanyia ushauri.

Mkufunzi atengeneze jukwaa kwa ajili ya wanachuo kufanya:
a)      Mazoezi ya ushauri kwa njia ya kuigiza kwa kufuata kanuni zote za ushauri wa Kikristo


Je, mwanachuo anao uwezo wa kushauriana au kupokea ushauri?


b)      Ushauri wa Kichungaji kwa jamii.
Mwanachuo aweze:
·        Kutoa huduma si kwa wakristo bali hata jamii inayomzunguka katika maswala mbalimbali ya ya jamii husika.
Mkufunzi asisitize:
·        Umuhimu wa mchungaji kuisoma jamii anapo hudumia na kisha kuishi kati yao.
·        Kuruhusu kuingiliana kwa mema na wanajamii ili kuwapa nafasi ya kutaka msaada toka kwa mtumishi wa Mungu.

Je, mwanachuo anaweza kumshauri mtu asiye wa imani yake?

PT303
UONGOZI NA UTAWALA WA KANISA
1.      Maana ya uongozi na utawalaa.










2.      Utawala wa Kanisa

3.      Mahusiano na viongozi wengine wa makanisa na makundi mbalimbali katika jamii.












Mwanachuo aweze:
·        Kueleza kwa ufasaha maana ya uongozi na utawala
·        Kutoa tofauti za zilizopo katika ya uongozi na utawala
·        Kuelezewa aina za uongozi na utawala.
·        Kujitambua kuwa ni meneja wa parish na mtaalam wa fani yake.
·        Kuwa na uhusiano na madaraja mengine ya utawala wa kanisa na jamii pia

Mkufunzi awaongoze wanachuo:
·        Kujadili maana na aina za uongozi na utawala
·        Kujadili falsafa mbali mbali juu ya uongozi na utawala
·        Kujadili sifa za kiongozi bora
·        Kujadili utawala wa Kibiblia
·        Kuchora na kujadili utawala wa kanisa
·        Kujenga hali ya mwanachuo kuheshimu uongozi ulio juu yake.
·        Kumtambulisha mwanachuo kuwa ni kiongozi katika kada yake.
·        Kwa kutumia Katiba ya Dayosisi na Kitabu cha Mapasta kuonyesha mipaka ya kiuongozi

Je, mwanachuo ni mahiri kwenye uongozi na utawala wa kanisa lake?





Je, hali ya mwanachuo kuheshimu watawala na viongozi wengine wa kanisa unaridhisha kuwa kiongozi bora wa kanisa?


Je, mwanachuo anamtazamo gani katika utawala wa sasa wa kanisa, mchango wake nini?
45
PT313 UTAWALA WA FEDHA
·         Maana ya utawala wa fedha

·         Vyanzo vya mapato ya kanisa

·         Uwakili (sadaka, Zaka, na changizo mbalimbali)
a)       
Mwanachuo aweze:
·        Kueleza kwa ufasaha juu ya utawala wa fedha
·        Kujadili umuhimu wa fedha katika matumizi ya kazi
·        Kuwa mbunifu katika kulipatia kanisa lake mapato
·        Kuwa wakili mwaminifu na kuwafundisha wengine uwakili

·        Kuleza na kusimamia vyema ulipwaji wa posho na akiba ya uzeeni (PF) yake
·         
Mkufunzi awaongoze wanachuo:
·        Kujadili maana ya utawala wa fedha.

·        Kuandaa utaratibu wa ukusanyaji na usimamiaji wa fedha za kanisa

·        Kutengeneza budget inayotekelezeka kwa kutumia vipaumbele vya wakati husika.

·        Kuonyesha au kuandaa vitabu vyote vipasavyo kuandakia fedha: mapato na matumizi.

·        Kuweka misingi ya uwakili kwa wachungaji.

·        Kuandaa taarifa za fedha katika shughuli mbalimbali za kanisa: miradi, matumizi mengine ya kila siku


30
MARUDIO YA MAHUBIRI
Vitendo tu.
Mwanachuo aweze:
a)      Kuandaa mazingira yake mwenyewe ya kuhubiri Injili.
b)     Kuhubiri katika ibada, familia, mikutano ya kiroho, na kuongoza semina.
Mkufunzi asimamie:
·        Mazoezi ya vitendo ya kuhubiri katika mazingira mbalimbali na kupima kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa mazoezi hayo
·        Kuwashauri wanachuo namna ya kufanya vizuri zaidi.


15

Muda wa ziada: Muhimu sana. Mkufunzi apange ratiba ya mahubiri kabla ya kuanza kwa semester kutoshereza muda wote wa semester na lengo kusudiwa.





























CH107 HISTORIA YA KANISA
Lengo la kozi hii ni ya muda wa kosi tatu ili kumfanya mwanchuo aelewe jinsi kanisa lilivyoingia Afrika na mchango wa bara hili katika kuhifadhi na kupeleka Injili kwa mataifa yote.

Mwisho wa kozi hii mwanachuo atakuwa na uwezo wa:
·         Kuelewa chimbuko la kanisa Afrika na historia yake
·         Kulinganisha hali halisi katika kanisa la leo na historia yake
·         Kuelewa changamoto ndani ya kanisa na jinsi ya kukabiliana nazo kulingana na wakati.
Kuelewa na kuchanganua kati ya kanisa la wakoloni na kanisa la Afrika ( Colonial church and African church).

Mambo muhimu kwa mwanachuo kufanya katika kozi hii
Mwanachuo anatakiwa kuhudhuria na kushiriki katika jumla ya vipindi 180 kwa miaka yote mitatu. Kila semester mwanachuo anatakiwa kukamilisha vipindi 45
Kila semester aandike insha mbili: moja binafsi na nyingine kwa makundi ambayo itawakilishwa kwenye semina kabla ya kukusanywa kwa mkufunzi.
Mwanachua atafanya majaribio yasiyopungua mawili kwa kila semester

MADA
KUU
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
HISTORIA YA KANISA

a)    Historia ya kanisa baada ya tangu Mitume hadi 1000BK
Mwanachuo aweze kuelewa
1. Mafundisho ya msingi, chimbuko na jinsi kanisa lilivyokuwa katika nyakati za awali.
Mkufunzi awaongoze wanachuo;
1. Kusoma vitabu vya historia ya kanisa tangu mitume hadi 1000BK



Je Mwanachuo ameweza kuelewa
Chimbuko la kanisa na jinsi lilivyokua na kuenea?

 b) Utangulizi wa historia ya kanisa Afrika
Mwanachuo aweze;
1.    Kuelewa jinsi ukristo ulivyoingia Afrika, na jinsi ilivyoenea katika nyakati za awali.
2.    Mababa wa kanisa hasa Waafrika; Augustine, Origen, Tertulian, Atanasia, nk.
Mkufunzi awaongoze wanachuo
1.    Kusoma vitabu vya historia ya ukristo Afrika.
2.    Kuchambua mafundiso na misimamo ya kiimani ya mababa wa imani Afrika

Je, mwanachuo ameelewa mafundisho makuu ya kihistoria ya kikristo









c)  Historia ya Ukristo Afrika Magharibi na Kati


Mwanachuo aweze kuelewa:
1.    Utangulizi, historian a kuenea kwa Ukristo Afrika Magharibi na Kati.
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:
1.    Kusoma na kujadili mbinu zilizotumiwa kueneza Ukristo na jinsi kanisa lilivyokua na linavyoendelea kukua huko hadi sasa.


Je, mwanachuo ameweza kuelewa njia kuu zilizotumika kueneza ukristo Magharibi mwa Afrika?
20
d) Historia ya Ukristo Afrika Mashariki





Mwanachuo aweze:
1.    Kuelewa historia ya Ukristo A. Mashariki
Mkufunzi awaelekeze wanachuo:
1.    Kusoma, Kujadili na kuchambua mbinu za uinjilisti zilizotumiwa kueneza ukristo katika Pwani ya Masharik ya Afrika.



Je, mwanachuo ameweza kuelewa historia ya ukristo na changamoto zake hasa katika eneo hili la Afrika Mashariki?
12

(e) Historia ya K. A. T

















Mwanachuo aweze kuelewa
1.      Historia ya Kanisa la Anglikana Tanzania.
2.      Mapokeo ndani ya KAT.
Mkufunzi awaongoze wanachuo:-
1.      Kusoma na kuchambua historia ya KAT.
2.      Kuangalia muundo wa uongozi, madayosisi na maendeleo ya KAT.


Je mwanachuo ameelewa;
1.      Historia ya KAT Kiasi cha kuielezea kwa ufasaha?
2.      Je ameelewa historiana muundo wa uongozi ndani ya KAT?












DD108 UTUME
Kosi imeundwa ili kumwezesha mwanachuo kujifunza mambo ya msingi sana yahusuyo huduma ya kiroho na kimwili (Holistic approach)

Mwisho wa kosi mwanachuo atakuwa na uwezo wa:
·         Kueleza maana ya Injili
·         Kujadili jinsi mamlaka ya Mungu na wajibu wa mwanadamu unavyotegemeana.
·         Kufikisha Injili kwa wasioamini.
·         Kubuni na kusimamia miradi binafsi na kanisa.
·         Kuandika mchanganuo wa mradi na utandaaji wa taarifa za miradi.
Kuwa mjasiliamali katika mtazamo wa kikristo hasa katika fani itakayojifunza na pia kuwa na eneo pana la kufikiri na kutekeleza maamuzi yake.
MADA KUU
MADA NDOGO
LENGO MAHUSUSI
MPANGO WA UFUNDISHAJI/KUJIFUNZA
ZANA ZA KUFUNDISHIA/
KUJIFUNZIA
TATHMINI
IDADI YA VIPINDI
UTUME NA MAENDELEO
a) Utangulizi wa Utume/Uinjilisti
Mwanachuo aweze kuelewa chimbuko na historia ya mada hii
Mkufunzi amwongoze mwanachuo kusoma na kujadili dhima ya mada hii, na jinsi kuitumia kwa sasa

Je mwanachuo ameelewa chimbuko la Utume/Uinjilisti?
Je mwanachuo anweza kuwa mtume na Mwinjilisti katika kanisa la sasa?


b) Uinjilisti na Maendeleo ya Kanisa
Mwanachuo aweze kuelewa umuhimu, mchango, na kazi ya Uinjilisti endelevu katika kanisa
Mkufunzi amwongoze mwanachuo Kusoma vitabu vya Uinjilisti, kuchambua, kulinganisha na kuangalia Filosofia mbalimbali za uinjilisti.

Je Mwanachuo anaweza kufanya Uinjilisti kulingana na Mazingira ya sasa?


c) Elimu ya Maendeleo:
Utangulizi, Maana, Umuhimu na Namna ya kufikia Maendeleo
Mwanachuo aweze kuelewa tafsiri, maana na jinsi ya kufikia maendeleo endelevu katika kanisa na jamii kwa ujumla
Mkufunzi amwongoze mwanachuo kusoma na kuchambua dhana mbalimbali za kimaendeleo na jinsi ya kuendelea, kujiendeleza na kuwaendeleza wengine.

Je mwanachuo ameweza kuelewa maana ya maendeleo?


d) Makisio (mapato na matumizi) Budget
Mwanachuo aweze kuelewa maana, aina za budget na jinsi ya kuandaa budget ya mwaka katika kanisa
Mkufunzi amwongoze mwanachuo kusoma, kujadili na kuchambua vipengele vya budget kulingana na aina ya budget. Pamoja na jinsi ya kusimamia budget

Je mwanachuo ameweza kuelewa maana ya budget, jinsi ya kuiandaa na namna ya kusimamia budget ya kanisa?


e) Andiko la Mradi
Mwanachuo aweze kuelewa maana na jinsi ya kuandaa Andiko la Mradi.
Mkufunzi amwongoze mwanachuo kusoma theory mbalimbali za andiko la mradi/miradi.

Pia Mkufunzi amwongoze mwanachuo kupitia kwa makini vipengele vya andiko la mradi na jinsi ya kuuza andiko lolote la mradi kwa wahisani

Je Mwanachuo ameweza kuelewa dhana mbalimbali za andiko la mradi/miradi?
Je mwanachuo anaweza kuandaa andiko la mradi wa maendeleo la kanisa?


f) Elimu ya Ufundi: Useremala/Ushonaji
Mwanachuo aweze kupata ujuzi na maarifa katika Ushonaji/Useremala, kwa ufanisi wa huduma yake kanisani
Mkufunzi wa Ushonaji/Useremala amwongoze mwanachuo kuelewa hatua zote za msingi za kiufundi kinadharia na kivitendo.

Je mwanachuo wa kosi ya Ushonaji anaweza kupima, kukata na kuunganisha nguo katika mitindo mbalimbali?
Je mwanachuo wa kosi ya Useremala anaweza kupima, kukata, kuranda na kuunda samani ya aina zote alizofundishwa?


1 comment:

  1. Very nice planning by Pastor Noah, Msalato Theological College

    ReplyDelete