SWALI: ONYESHA UHALISIA WALUGHA NA ISHARA ZILIZOTUMIKA KUELEZA IMANI YA KIKRISTO KUPITIA KWA BARUA KWA MAKANISA SABA.
UTANGULIZI
Imani ya kikristo imeelezwa kwa lugha, picha, ishara pamoja na alama mbalimbali katika Biblia. Mtumishi wa Mungu Yohana alifunuliwa mafunuo juu ya makanisa saba yaliyoko katika jimbo la Asia katika utawala wa kirumi, jinsi ya kuyaonya na kuyafundisha. Kila kanisa lilionywa kutokana na matendo yake, lakini mafundisho na maonyo hayo hayakuwa kwa makanisa saba tu bali ni kwa makanisa yote ulimwenguni (Ufunuo 3:13 taz. Mst. 22. sisi tutazungumzia uhalisia wa lugha na ishara zilizotumika kuelezea imani ya kikristo kupitia kwa makanisa saba.
KANISA LA EFESO
Mwanzoni katika kanisa hili watu wa Efeso wanasifiwa sana juu ya uwezo waliokuwa nao (Ufu. 2:1-3) lakini wanaonywa sababu ya kujiinua. Hapa lugha ya ishara iliyoonekana katika kanisa hili ni kinara, kwa uhalisi ni kujiinua, hivyo Mungu amewaonya watubu tofauti na hapo atakiondoa kinara hicho.
KANISA LA SMIRNA
Kanisa hili la Smirna lilipitia mateso mengi kwa sababu ya imani yao, mateso hayo yalisababishwa na wayahudi ambao walijiita wa kiroho kumbe siyo (Sinagogi la shetani), na picha kubwa inayoonekana hapa ni alama ya ushindi ambayo wataupata kwa kumwamini Yesu Kristo ambaye alikufa na kufufuka.
KANISA LA PERGAMO
Japokuwa kanisa hili la Pergamo lilidumu katika neno la Mungu (upanga), lakini wapo watu ambao walileta mafundisho ya uzushi ambao ni wanikolai waliojenga mafundisho yao juu ya sanamu na walitaka wakristo washiriki ibada hizo. Hapa tunaona ishara ni jiwe jeupe linaloashiria Baraka.
KANISA LA THIATIRA
Hili ni kanisa linalozungumuza na Kristo mwana wa Mungu, limeshika maagizo na kuyatenda, lakini limeruhusu matendo yasiyofaa kama uzinzi, lugha na ishara ni uzinzi na uhalisia wake ni kumkataa Mungu na kufuata mambo yasiyofaa na wanaagizwa kutubu.
KANISA LA SARDI
Kanisa hili linatamkwa kama kanisa lililokufa lakini linatarajiwa kuwa hai. Pia halikuwa na tatizo lolote na halikuwa na mafundisho yoyote ya uongo wala mateso.Hivyo lilienda katika njia nyoofu (Ufu. 3:9) “kinachohitajika hapa ni uhamsho wa imani” lugha na ishara ni kuvishwa mavazi meupe ambayo uhalisia wake ni kutakaswa na kuhakikishwa (tunatakaswa duniani, tunahakikishwa mbinguni).
KANISA LA FILADELFIA
Kanisa lililotunza imani. Linaanza kwa kumtangaza Yesu na lililosimama katika imani yake, na linatoa unabii kuwa Yesu ndiye Masihi atokaye katika uzao wa Daudi.Yesu anawapa uwezo wa kiimani ambayo hakuna anayeweza kuiondoa japo kuna sinagogi la shetani (walioabudu miungu) kutokana na imani yao hao nao watageuzwa na kumwamini Yesu Kristo. Pia wameahidiwa yerusalemu mpya itakayoshuka kutoka mbinguni. Hii ni ishara na lugha ambayo uhalisia wake ni ufalme wa Yesu Kristo.
KANISA LA LAODIKIA
Hili ni kanisa lililojiona kuwa ni timilifu kutokana na mali waliyokuwa nayo. Lakini machoni pa Yesu walikuwa vipofu pia walikuwa uchi. Yesu anawahitaji warudi kwake ili watubu wapate kuona na wavishwe mavazi na kuwapa dhahabu iliyosafishwa kwa moto. Lugha na ishara hapa ni upofu na uchi na kuwa vuguvugu, uhalisia ni umaskini wa kiroho.
HITIMISHO
Hizo zote hazikuwa barua kwa makanisa hayo bali zilikuwa ni ishara na lugha kwa sababu Yohana alikuwa katika kisiwa cha Patmo na huo ulikuwa ni ufunuo kwake. Hivyo mafundisho haya ni msaada kwa makanisa/kanisa la leo. Lakini baada ya kuyaona na kujifunza, mafundisho hayo ni vizuri kufikia hitimisho kwamba “tufungue mioyo yetu Yesu aweze kuingia na kufanya makao ndani yetu na kutuongoza katika hali ya maisha ya kiroho” (Ufu. 3:20, 2)
WAHUSIKA WA KIKUNDI
Magret Kasanda
Samson Albert
Samwel Nguti
Samwel Ntungilija
Emmanuel Kazoba
Paulina Nyang’ombe
Fabian Bahati
MAONI YA MWALIMU
1. Kwa ujumla kazi yenu ni nzuri sana.
2. Ulinganishaji wa ishara na ufafanuzi umeendana na na hitaji la kazi
3. Alama:
78%
No comments:
Post a Comment