SWALI: ONYESHA UHALISI WA LUGHA ISHARA ZILIZOTUMIKA KUELEZEA IMANI YA KIKRISTO KUPITIA KWA BARUA SABA KWA MAKAN IS A SABA.
MAPITO YA IMANI
Katika mapito ya imani mara nyingi kanisa linakumbana na changamoto mbalimbali kama tulinyoona katika makanisa saba[2] yalinyoweza kukumbana na changamoto za mafundisho ya uongo yaliopelekea kupotosha imani zao na kugeukia mafundisho haya yasiyokuwa ya imani itokayo kwa Mungu[3] . Kwa hali hiyo barua hizo ziliwatia moyo na kuwa faraja kwao kutokana na majeraha waliyoyapata kupitia mafundisho ya uongo kwa kipindi hicho wakristo wengi walijeruhiwa.
HATUA ZA IMANI
Katika makanisa haya saba kwa barua hizo ziliwakumbusha kumrudia Mungu wao na kuona ukweli wa neno la Mungu, kuwa wanatakiwa kutazama nyuma na kuangalia mbele na waishi sasa (Uf 2:5)[4]
Tunachojifunza kuhusu barua za makanisa saba yaliyopo katika kitabu cha ufunuo ni UVUMILIVU NA UNYENYEKEVU[5], katika imani na kujenga imani iliyo dhabiti katika uwepo wa Mungu na kuwa na tumaini la uzima wa milee.Katika barua hizi tunakumbushwa kutazama nyuma kuangalia mbele na kuishi sasa.
MAONI YA MKUFUNZI:
WAHUSIKA WA KIKUNDI
- YOHANA KALIKI
- CELESTINE RABANI
- NEEMA ANDREA
- MARKO BUNKWIMBA
- DANIEL OPUDO
[1] Hakuna utangulizi unaofanana na hitaji la swali (alama
[2] Mlitakiwa kujadili kwa kina ishara na lugha mbali mbali katika kifungu cha maandiko mlichopewa. Tofauti yake mnatoa taarifa ya nini mlichofundishwa.
[3] Ni sawa, lakini unapopewa kazi ya insha, tafadhali tambua wapi pa kuandika nini. Wazo hilo lilitakiwa kuwa kwenye hitimisho.
[4] Katika sehemu (aya) hii mmejaribu kukusanya mawazo yote na kuandika kwa ufupi. Lengo la kazi hii haikuwa na kusudi hilo. Ulitakiwa kueleza lugha za ishara zote zinazo patikana katika barua za makanisa yote saba na kisha kujibu kwa namna gani imani ya kikristo inanufaika na barua hizo hasa katika ulimwengu wa sasa.
[5] Haya ni baadhi tu ya mafundisho ya kikristo yapatikanayo katika barua hizo. Kuna mafundisho mengine kama Upendo, Kutoshikamana na dhambi, Kutenda haki nk.
MAONI YA UJUMLA:
Kazi hii siyo ya kitaaluma: Mlitakiwa kuonyesha kwa ufupi lengo la barua, lugha au ishara zinazotumiwa na mwandishi kisha kuziweka bayana ufaidishaji katika kanisa leo.
No comments:
Post a Comment